Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: msemaji mkuu wa wizara ya mambo ya nje wa Ujerumani aliyasema hayo katika maojiano alioyafanya siku ya Jumatatu na mawakala wa vyombo vya habari vya kimataifa katika mji mkuu wa Ujerumani (Berlin) kwamba: waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani (Frank Meyer) alikuwa katika mazungumzo ya masaa 3 mjni London siku ya Jumamosi wakipitia mitazamo ya mawazi wenzake wa Ufaransa, Uwingereza na Marekani kuhusu njia ziliopo zakufikia muafaka wa kideplomasia na Iran.
Martin Schaefer alisema pamoja yakuwa timu ya mazungo ya mpango wa nyukilia wa Iran umepiga hatua ya maamuzi mazito katika suala hilo ama muafaka wakaribia kufikiwa, aidha akinukuu kutoka kwa Frank Meyer Alisema: toka tulipoanza mazungumzo hatukuwa tumefikia hatua tulioifikia sasa, kwani tumepiga hatua kubwa sana za matumaini katika mazungumzo ya wiki iliopita.
Mazungumzo ya mwesho baina ya Iran na kikundi cha 5+1 kiliisha siku ya ijumaa iliopita ambacho kiliofanyika katika mji mkuu wa Uswisi, na utarudiwa tena siku ya Alhamisi ya wiki hii hukohuko nchini Uswisi.
Iran na kikundi cha 5+1 kinachokusanya nchi zifuatazo Marekani, Uwingereza, Urusi, Ufaransa, China na Ujerumani ambapo wanatakiwa mpaka tarehe 30 juni kufikia muafaka huo.
23 Machi 2015 - 20:20
Msimbo wa Habari: 678620
Msemaji mkuu wa wizara ya mambo ya nje wa Ujerumani amesisitiza kuwa Iran na nchi 6 zenye nguvu Duniani wako katika hali ya kufikia makubaliano ya kisiasa katika mazungiumzo ya mpango wa nyukilia wa Iran